Sikiliza Mchezo wa Redio wa Wahapahapa na Ushinde Muda wa Maongezi Kila...
Soma zaidi
Hadithi ya Upanga
Upanga ni eneo muhimu sana katika historia ya muziki Tanzania. Hata katika miaka ya karibuni kulizuka kilichoitwa East Coast, muungano fulani wa...
Soma zaidi
MWAMBA NGOMA: Filamu ya Kitanzania Kuwania Tuzo za Filamu Afrika
Tanzania imefanikiwa kuingiza filamu yake yenye mfumo wa jarida (documentary) inayokwenda kwa jina la "Mwamba Ngoma" katika kinyan’ganyiro kikali cha tuzo za filamu Afrika huko nchini Nigeria (AMAA) yani African Movie Academy Award.
Tamasha hilo la utoaji wa tuzo za filamu litafanyika jumamosi hii ya mwezi wa nne nchini Nigeria, Na kwa hapa nchini jarida hilo litaonyeshwa siku hiyo hiyo na televisheni ya channel 5 saa 3 usiku ama pia kwa sasa unaweza kuona vidokezi vyake katika tovuti yao ya www.wahapahapa.com
Jarida hilo hapa nchini limetayarishwa na kampuni ya MFDI yenye kuhusika na utangazaji wa habari za maendeleo ya jamii kwa kutumia vyombo vya habari nchini na nje ya nchi. Jarida hilo limetengenezwa likihusisha habari za muziki na maisha ya wanamuziki tofauti tofauti wa hapa nyumbani juu ya maisha yao ndani na nje ya muziki huo huku wakiweka na vionjo tofauti juu ya utayarishaji uliokuwa ukifanyika juu ya video za muziki wa albamu nzima ya mseto wa wahapahapa iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya elimu ya sanaa ya muziki na maambukizi ya ukimwi.
Kati ya video zilizomo kwenye mseto huo na pia kuonekana katika jarida hilo ni pamoja na ile video ya Banana Zoro ya 'Zoba', Lady Jay Dee na 'Shamba', Enika na "Changanyachanganya", Mzee Yusuph na 'Mtoto wa Matumaini', na wengine wengi. Jarida zinazowania nafasi moja pamoja na Mwamba Ngoma ni pamoja na Peace Wanted Alive ya nchini Kenya, Baringa Boys kutoka Nigeria, En quette d’identite ya nchini Bukina Faso na Innovating Africa kutoka Nigeria.
Tamasha hilo la utoaji wa tuzo utafanyika hapo jumamosi ya mwezi wa nne huko huko nchini Nigeria, lakini hapa nchini jarida hilo litaonyeshwa siku hiyohiyo na televisheni ya channel 5 saa 3 usiku.