Orodhesha anuani yako ya barua pepe kupata habari:



 

 
 

Sikiliza Mchezo wa Redio wa Wahapahapa na Ushinde Muda wa Maongezi Kila... Soma zaidi

 

 

Hadithi ya Upanga

Upanga ni eneo muhimu sana katika historia ya muziki Tanzania. Hata katika miaka ya karibuni kulizuka kilichoitwa East Coast, muungano fulani wa... Soma zaidi

Ona Zaidi

 




 

Kulikoni Suzuki na Extra Bongo?

Si nyingine bali ni ile bendi ya muziki wa dansi ya Extra Bongo 'Next Level', haikuweza kufanikiwa kuingiza wimbo wa 'Mapenzi Sio Pesa' kwenye albamu ya kwanza ya 'Mjini Mipango'.

Kibao hicho ni cha mwimbaji wake wa zamani Seleman Ramadhan 'Suzuki', kwa sasa mwimbaji huyo amerudi kwenye bendi yake ya zamani ya Levent Musica yenye maskani yake mjini Morogoro.

Naye Mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki alisema kwamba wimbo huo haumo kwenye albamu hiyo, na badala yake itawekwa kwenye albamu nyingine ingawa ni moja ya mipini ya mwanzoni ya bendi hiyo.

Alisema mpaka sasa hawajaweka albamu hiyo labda hapo badae, watakapoandaa albamu ya pili kwani kwa sasa haumo na tayari albamu imesheheni nyimbo za kutosha.

Baadhi ya mipini ya albamu hiyo ya 'Mjini Mipango' ni pamoja na 'Maisha Taiti', 'Laptop', 'Safari ya Maisha', 'Wema', 'Niacheni' na 'First Lady'.

Choki alisema wimbo wa Mapenzi siyo pesa ni mali ya bendi hiyo, kwani watatafuta uwezekano wa kuuweka kwenye albamu hiyo.

Kwa sasa bendi hiyo inaendelea kujianika kwa mashabiki wa miondoko ya dansi wa mikoa mbalimbali hapa nchini, na ilianza kufanya vitu vyake visiwani Zanzibar, Iringa, Mbeya ikiwemo na Morogoro.

 


 



>> Ona Zaidi

 

 
  1. Pancho/Mx Carter/Mabeste/Leo/Izzo B...
    We Go Harder
  2. AT/Nyota Ndogo
    Mpishi
  3. Blac/AT/Gelly/Rose
    Hood Life, Good Life
  4. AT/Gelly
    Waswahili
  5. Soma zaidi
 
 
Nuru

Kuna shabiki wa muziki aliwahi kuniambia kwamba, 'Nuru is sooooo marketable', kwa maana nyingine amekamilika katika Soma zaidi