Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
Nyota wa Filamu Anayekimbiza Wakongwe

Akiwa bado kijana mdogo Mlela ameweza kuuteka ulimwengu wa sanaa  akiwapiku wakongwe wengi ambao wamekuwa katika tasnia ya maigizo kwa muda mrefu alianza kutamba 2006 alicheza filamu  iliyoitwa ‘Diversion of Love’ kupitia kampuni ya Mtitu. Ndani ya filamu hiyo alicheza kama muhusika mkuu katika filamu hiyo kwa jina la James. Hakika ilikuwa filamu aliyoipenda kati ya filamu 20 alizowahi kucheza kwani ilikuwa ni ya kwanza na hakuwa na uwezo mkubwa wa kucheza na aliicheza na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Filamu hiyo ilimwezesha kuibuka mshindi wa tuzo ya msanii bora Chipukizi katika uigizaji mwaka 2008. Mlela anasema hakuna bahati au upendeleo ili kupata mafanikio katika sanaa zaidi ya  kujituma na kujali kazi yako, kutengeneza msingi imara ili usitetereshwe na misukosuko mingi iliyopo katika tasnia hiyo.


Ukimtaja Mlela kutokana na filamu kali alizocheza bila shaka kwa wadau wa filamu watamtambua hasa kwa Filamu yake ya kwanza iliyoanza kumpatia umaarufu.

Jina lake la kuzaliwa ni Yusuph Godfrey Mlela na hujulikana kwa jina la Angelo na alizaliwa Oktoba 11, 1986 na ni mzaliwa za Tabora.

Kazi anazofanya ni Uigizaji, Mwanamitindo,Mtunzi wa filamuMwaka aliojikita kwenye Filamu ni 2006 nmpaka kufikia sasa.

Elimu yake ya Shule ya msingi aliipata katika shule ya Kumbukumbu iliyoko Kinondoni hapa Jijini na baada ya hapo nilijiunga na Secondary Kawawa iliyoko Mafinga mkoani Iringa ambapo alisoma mpaka kidato cha nne, kisha akasomea nikasoma masuala ya Compyuta.

Yusuph alisema kuwa alipoona anaweza kujikita katika Filamu akaamua kijiunga katika kikundi cha maigizo cha Tanganyika ambapo alikuwa akichukua mazoezi huko hakukaa kwa muda mrefu kwani mbali na shughuri hiyo alikuwa akijishughurisha na mambo ya mitindo katika fasheni shoo.

Mpaka kufikia sasa amecheza Filamu Ishirini na mbili lakini filamu alizofanikiwa kutoka ni kama ifuatavyo.. Division Of Love, The Blind Side of Marriage, Man Desire, Secretary, Death Race, April Fool, Times Goes Around, Its Too late, Last Minits, Divorce, September 11,Tax Driver, Miracle of Love, September 11.

Akiongelea matarajio yake ya baadae “Natarajia kuwa muigizaji wa kimataifa kwani mpaka sasa nimeshaanza mazungumzo na wasanii wa nje akiwemo Wandeb wa Afrika kusini aliyewahi kucheza filamu ya Coming Home”

Mlela akipewa nafasi ya kutoa ushauri kwa wasanii wenzake anasema kuwa”Nawashauri wasanii wenzangu walioingia kwenye Game wasikate tamaa kwani Game ni ngumu sana, kuna vikwazo vingi kuna watu wanaopenda na kuna watu utakutana nao wasiopenda wewe uendelee, nawashauri wasikubali wapigane kwani hakuna kisichowezekana.

Akielezea mafanikio yake katika sanaa, Mlela anasema tasnia hiyo inalipa kiasi fulani na sasa hivi  imekuwa ni ajira kwani angalau baadhi ya watu wazee kwa vijana wamekuwa wakijipatia kipato na maisha yamekuwa tofauti na zamani. “Sasa hivi  vijana na hata wazee wa hapa Tanzania wanaitegemea sanaa ya maigizo kuwaingizia kipato. Kampuni ya Mtitu imewafanya waone sanaa kama ajira.

Alisema hata yeye imemsaidia kwani anaweza kuisaidia hata familia yake na kuweza kutatua matatizo madogomadogo.

Mlela alisema ndani ya tasnia hii kinachomkwaza ni wizi wa kazi za wasanii. Hilo limekuwa likiwarudisha  sana nyuma wasanii wa filamu.

Na changamoto nyingine inayomuweka Mlela katika wakati mgumu ni majungu miongoni mwa wasanii, alisema Sanaa hii inaonekana kama ya kihuni kutokana na wasanii kusengenyana na kuoneana wivu.

Alisema majungu yamezidi miongoni mwao kwani baadhi ya wasanii wakikuona umefanikiwa  wanaanza kukusema vibaya; kwa ujumla hawapendi kuona upo juu kimaisha.

Mlela ana ndoto ambazo anataka kuzitimiza, kama ilivyo kwa binadamu yoyote mwenye utashi anatamani  kufikia kilele cha mafanikio na anaahidi kufanya juhudi za dhati kuyafikia malengo hayo.

“Kwanza kabisa ili niyafikie mafanikio hayo nataka nitengeneze Blog yangu, ambayo itakuwa inatoa taarifa na mipango yangu ya kimaendeleo kwa vijana. Pia nitatumia kipaji changu ili siku moja nicheze filamu na Slyvester Stalone (Rambo),”anabainisha Mlela.


Yajuye Mambo matano kuhusu Yusuph Godfrey Mlela: *Alisoma Shule ya Sekondari Kawawa iliyopo Mafinga, mkoani Iringa. *Alisoma shule ya msingi kumbukumbu *Ana mchumba anayetarajia kumuoa siku za hivi karibuni *Anapenda kuvaa vizuri ili kuonekana mtanashati.         

Mwisho Mlela alisema kuwa katika Filamu ambazo anazipenda sana ni pamoja na Division of Love filamu ambayo ilimfungulia ukurasa na kama akiambiwa ni filamu ipi irudiwe kuchezwa ataitaja Blind Side Of Marriage kwani katika mlolongo wa filamu nzuri ambayo alishakuwa staa wa movie ni pamoja na hiyo.

Habari na Sia John

 

Maoni  

 
0 #2 Masoud Seleman 2010-11-22 06:10
Hongereni sana kwa ubunifu wenu na mzidishe juhudi kwani mnatusaidia kujua ukweli kuliko kusoma kwenye magazeti ya udaku.
 
 
0 #1 dany aza macheda 2010-11-20 10:30
Nawapongeza wale wote waliofanikisha tovuti hii kuwepo.Kwakweli mmefanya kazi nzuri na mnatupa sisi nafasi ya kuyajua yale ambayo ingekuwa shida kwetu kuyajua bg up WAHAPAHapa
 

Weka Maoni

Security code
Upya

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.