Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
26 Mei 2011

CHUMO

CHUMO

Filamu ya chumo iliyotayarishwa hapa nyumbani Tanzania inazinduliwa rasmi  katika viwanja vya BIAFRA hapo juni tarehe 4 mwaka huu,
uzinduzi huo utakuwa ni wa bure kabisa na wenye burudani yakutosha, mbali na kuonyeshwa kwa filamu hiyo pia kutakuwa na burudani ya muziki kutoka kwa ASHIMBA na JAGWA MUSIC.

Filamu hii iliyo na misukosuko ya mapenzi na mafunzo tele tayari imeshaanza kuwika hata nje ya nchi kwani tayari imehsaingia kwenye
vinyanganyiro vingi tu.

Filamu ya Chumo imeshinda tuzo za Golden Hamster katika tamasha la filamu la Northwest Projections, Washington, Marekani. Filamu hiyo
iliyoongozwa na Jordan Riber, mtoto wa mtayarishaji wa filamu mkubwa Afrika aliyewahi kutamba na filamu ya NERIA,Chumo ilishindanishwa
pamoja na filamu nyingine ya makala nakushinda kama filamu bora fupi.

Nahapo hapo tayari Chumo imeteuliwa ZIFF kwani imechaguliwa kushiriki katika kinyang'anyiro cha tuzo za filamu za tamasha la ZIFF huko
Zanzibar. Tamasha la ZIFF litajiri kuanzi June 18 hadi 26, 2011. Kwa hayo tu ningependa kukushauri wewe kama mpenzi wa filamu za
kiafrika uhudhurie siku hii, kwani hii filamu sio zile tulizozoea kuziona za kuburuzwa buruzwa, hi ni filamu ambayo wewe mwenye kama
mtanzania utafurahia kujua kumbe hata nyumbani kazi nzuri inawezekana kufanyika.

Imetayarishwa Tanzania na kufadhiliwa na JHU-CCP kupitia Mfuko wa Rais wa kutokomeza Malaria na USAID. Chumo inawasilisha ujumbe wa malaria wakati wa ujauzito kupitia hadithi ya kusisimua ya wapenzi wenye bahati mbaya.

Malaria Haikubaliki.

Na Kulthum Maabad

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.