Malumbano kati ya Rais wa Masharobaro 'Bob Junior' na msanii Cyrill imechukua nafasi nyingine, baada ya Rais huyo kudai hamfahamu Cyrill. Aliyasema haya siku ya Jumanne alipofanya mazungumzo ya simu katika stesheni ya radio ya Clouds fm
Kupitia ukurasa wake wa Facebook mtu mzima Cyrill amempa kubwa Bob Junior
ambaye pia ni producer anayemiliki studio za Sharobaro Records iliyowatoa wasanii wengi tu.
Nanukuu....."Inawezekanaje kumtafuta mtu usiemjua?? alafu unafanya interview maelfu wanakusikiliza unasema humjui mtu uliyemuomba aje afanye track na wewe tena kwa kuomba kwelikweli....harufu ya umaaarufu inawaponza watu kama
hawa....kweli jamaa ana feli sana na hata kuifanya hiyo Sharobaro ichukuliwe kivingine.
Sina bifu na jamaaa nilikua nataka kusolve situation ya miaka mitatu nyuma na yeye ila nimegundua ni vigumu kusolve situation na sh*ga..
Noma hili lilianza baada ya Rais wa Masharobaro akiwa kwenye interview na kituo kimoja cha Radio kudai kuwa hamfahamu msanii yoyote anayeitwa Cyrill.