Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
04 Aprili 2011

Five Star Yaibuka na - Nimeitwa Mbele Yao

Five Star Yaibuka na - Nimeitwa Mbele Yao

Wimbo Mpya wa kuwaenzi wasanii 13 wa 5STAR waliofariki kwenye ajali mbaya hivi majuzi tayari umeanza kusikika kwenye redio mbalimbali,wimbo huo uitwao MBELE YAO umetungwa na mpiga kinanda wa siku nyingi bwana THABIT ABDUL na kuimbwa na wasani mbalimbali wa muziki huo wa taarab.

Msiba huo mkubwa ambao ulitikisa tasnia ya muziki nchini naku kosakosa wasani wakubwa nchini kama HADIJA KOPA, uliwaacha mamia wakililia ndugu na jamaa zao waliowatoka gafla.

Wasanii waliyoshiriki katika kuimba wimbo huo ni mwimbaji wa kundi la TOT, Mariam Khamisi ambaye zamani alikuwa 5’Star, Omary Tego wa kundi la Coast Taarab, Hadija Kopa wa TOT, Hassan Ally na Thabith mwenyewe.

Baadhi ya waimbaji waliokuwa wamejumuishwa kuimba ambao hawakuimba ni Mzee Yusuph, kiongozi wa kundi la JAHAZI, aliyesema kuwa dini yake haimruhusu kuimbia watu waliofariki, mwingine ni Mrisho MPoto aliyekuwa safarini nje ya nchi.

Habari na Kulthum Maabad

3 maoni

  • Maoni Jitu minofu 07 Aprili 2011 Jitu minofu

    Mzee yusuph dini yako inaruhusu kuimba taarabu?!

  • Maoni elly 06 Aprili 2011 elly

    yusufu amelowa umaarufu, so keshajiona super star na ambaye hawezi kushirikiana na wenzie

  • Maoni Sabiha 05 Aprili 2011 Sabiha

    Yusuf aache longolongo.....si useme ukiimba kwa kushirikiana promo unakosa!!!

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.